Текст Diamond Platnumz – Mapenzi Basi
Текст:
Mi mwenzenu tena basi
Oh mapenzi sitaki
Oh mwenzenu tena basi
Basi sitaki
Yalinifanya nikaugua
Mara napanga napangua
Mwili ukakonda nikapungua
Ah sikulala, sikulala
Oh maradhi nikaugua oh
Yakanichoma na kuungua roho
Kutwa nawaza na kuwazua
Sikulala
Hayo mapenzi bwana, hayana maana
Yalinifanya mi nichekwe
Sababu yake nshagombana, nikatukanwa
Lakini akanipiga teke
Ai haya mapenzi bwana, hayana maana
Yalinifanya mi nichekwe
Sababu yake nkagombana, usiku mchana
Yeye
Mi mwenzenu tena basi
Oh mapenzi sitaki
Oh mwenzenu tena basi
Basi sitaki
x2
Oh nilishagombana na mama mzazi
Akataka nimwagia radhi
Sababu yule fulani, yule wa moyo wangu
Yakaleta zengwe kwa kazi
Vurugu kwa majirani
Ah, ee Mola wangu
Hayo mapenzi bwana, hayana maana
Yalinifanya mi nichekwe
Sababu yake nshagombana, nikatukanwa
Lakini akanipiga teke
Ai haya mapenzi bwana, hayana maana
Yalinifanya mi nichekwe
Sababu yake nkagombana, usiku mchana
Yeye
Mi mwenzenu tena basi
Oh mapenzi sitaki
Oh mwenzenu tena basi
Basi sitaki
x2