GLyr

Diamond Platnumz – Upofu

Исполнители: Diamond Platnumz
обложка песни

Текст Diamond Platnumz – Upofu

Текст:

Mi kweli natamani siku iwezekane
Nifumbue macho mi kuona
Nijue sababu gani, unanipenda sana
Wakati siwezi mi kuona?

x2

Mara nyingi peke yangu nawaza
Namuomba Mungu nisije kukwaza
Nikaja kukupa maudhi na nafsi kuichoma
Chei, tena usiku mzima nalia darling
Napiga goti kwa Mola nasali
Azidi tupe baraka tusije kosa dona

Eh, mi macho yangu nimejaliwa mboni lakini nuru sina
Ningekuwa na uwezo ningefanya kazi nikuhudumie
Upofu wangu ndo kikwazo kikubwa, mwenzako raha sina
Lakini unanijali, mbali na mengi unanipenda sana

Mi kweli natamani siku iwezekane
Nifumbue macho mi kuona
Nijue sababu gani, unanipenda sana
Wakati siwezi mi kuona?
x2

Nasikia kuna rangi ya upendo
Ili upendwe kuna pozi za mwendo
Utanashati, udambudambu na urembo mi sina
Mi natamani nitazame
Kwa ardhi na mbingu nilalame
Nipande mawingu na niiname
Uwenda nikaona

Eh, mi macho yangu nimejaliwa mboni lakini nuru sina
Ningekuwa na uwezo ningefanya kazi nikuhudumie
Upofu wangu ndo kikwazo kikubwa, mwenzako raha sina

Lakini unanijali, mbali na mengi unanipenda sana

Mi kweli natamani siku iwezekane
Nifumbue macho mi kuona
Nijue sababu gani, unanipenda sana
Wakati siwezi mi kuona?
x2

Nikuone mama, niweze tazama
Every body say ee-eeh ee-eh ee
Ee-eh ee-eh ee, eh
Ee-eh ee-eh ee, I love you, nakupenda
Tena! Ee-eh ee-eh
Ee-eh ee-eh ee, eh
Ee-eh ee-eh ee, I love you, nakupenda
Say ee-eeh ee-eh ee
Ee-eh ee-eh ee, eh
Ee-eh ee-eh ee, I love you, nakupenda