Lyrics Diamond Platnumz – Mbagala
Text:
Busara na upole, na hekima nilorithi kutoka kwa mama yangu, mama
Vyote haukuvijali, ukaona silingani kabisa kuwa na wewe
Ka kuti na mkole, ukakata kabisa na shina la penzi langu nana
Eti kisa mali, ukaona bora uniache mimi na uolewe
Unavishwa pete unakuwa mke wa fulani
Nliumia sana, sana
Ile siku shekhe namuona anachoma ubani
Unavishwa pete unakua mke wa fulani
Niliumia sana, niliumia sana, sana
Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
Ungejua jinsi gani
Machozi nlolia kwa uchungu wa penzi langu na
Mwenzio jinsi gani, vile nimeumia moyoni
Hata kupendwa sitamani
Utamu wa mapenzi mwenzako umekula kwangu ma
Mwenzio sitamaani, hata raha tena mi sioni
Ah naskia hivi sasa una mtoto anaitwa Mamu
Vile akinuna mpaka atabasamu
Mmefanana sana, sana
Mi mwenzako tena mapenzi mi sina hamu
Tena na mpango wa kuhama Dar Es Salaam
Nataka niende mbali, niepuke vita na walimwengu
Mi mwenzenu siwezi
Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
Nasema Mbagala, Mbagala, Mbagala aa aaha
Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
Nasema Mbagala (Mbagala), Mbagala (Mbagala), Mbagala (Mbagala) ee eh