GLyr

Sauti Sol – Nerea

Singers: Sauti Sol
Albums: Sauti Sol – Live And Die In Afrika
song cover

Lyrics Sauti Sol – Nerea

Text:

Nakuomba Nerea, usitoe mimba yangu we
Mungu akileta mtoto, analeta saa ni yake
Mlete nitamlea, usitoe mimba yangu we
Mungu akileta mtoto, analeta saa ni yake

Huenda akawa Obama, atawale Amerika
Huenda akawa Lupita, Oscar nazo akashinda
Huenda akawa Wanyama, acheze soka Uingereza
Huenda akawa Kenyatta, mwanzilishi wa taifa

Nakuomba Nerea, usitoe mimba yangu we
Mungu akileta mtoto, analeta saa ni yake
Mlete aitamlea, usitoe mimba yangu we
Mungu akileta mtoto, analeta saa ni yake

Huenda akawa Maathai, ayalinde mazingira
Huenda akawa Makeba, nyimbo nzuri akatunga
Huenda akawa Nyerere, aongoze Tanzania
Huenda akawa Mandela, mkombozi wa taifa

Nakuomba Nerea, usitoe mimba yangu we
Mungu akileta mtoto, analeta saa ni yake
Mlete aitamlea, usitoe mimba yangu we
Mungu akileta mtoto, analeta saa ni yake

Nakuomba Nerea, Nerea, Nerea
Usitoe mimba yangu
Nerea, Nerea, Nerea
Usitoe mimba yangu

Huenda akawa Kagame (Atawale)
Jaramogi Odinga (Tuungane)
Huenda akawa Tom Mboya
Huenda akawa Rudisha
Huenda akawa Malaika, Mungu Ametupatia
Huenda akawa Sauti Sol

Huenda akawa Amos & Josh
Huenda akawa
Huenda akawa Malaika, Mungu ametupatia

Album

Sauti Sol – Live And Die In Afrika